Kiitalia
Kiitalia Italiano (it) |
|
---|---|
Lugha | |
Asili | Italia, San Marino, Uswisi (Ticino na Graubünden), Vatican |
Wasemaji |
L1 : 65 Milioni |
Familia za lugha | Kihindi-Kiulaya Kilatini Kirumi Kiitalia-Kidalmati Kiitalia |
Aina za Awali | Kilatini cha Kale Kilatini Halisi Kituscan Kiflorentia |
Mfumo wa kuandika | Alfabeti ya Kilatini |
Lugha Rasmi | |
Lugha rasmi kwa | Nchi 4 |
Nambari za Msimbo | |
ISO 639-1 | it |
ISO 639-2 | ita |
Glottolog | ital1282 |
![]() Lugha ya Kiitalia na uenezi wake |
Kiitalia ("lingua italiana" au "italiano") ni lugha ya kirumi katika lugha za Kihindi-Kiulaya na ndiyo iliyo karibu sana na lugha ya Kilatini.Ikiwa na wasemaji milioni 85 ambao Milioni 67 kama lugha ya mama ni lugha ya 21 kubwa zaidi duniani.Ni lugha rasmi ya Italia, San Marino, Vatikano, Uswisi na katika sehemu za Slovenia na Kroatia.Inatumika pia katika Monako, Malta, Albania na visiwa kadhaa vya Ugiriki), halafu bado katika elimu katika nchi zilizokuwa makoloni ya Italia kama Eritrea, Libya, Ethiopia na Somalia.
Watu wengi wanaokitumia kama lugha mama wamekisambaza katika nchi zote walikohamia, kama vile Ujerumani, Ufaransa, Ubelgiji, Marekani, Kanada, Brazil, Uruguay, Argentina, Venezuela, Australia n.k.[1]
Ni ya 4 kati ya lugha za kigeni zinazosomwa zaidi duniani, hasa kwa sababu ya umuhimu wake katika ustaarabu, kuanzia muziki, lakini pia katika biashara, k.mf. ya bidhaa za utamaduni wa Italia.
Kihistoria asili yake ni lugha ya Kilatini, hivyo pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania na lugha nyingine ndogo ni moja ya lugha za Kirumi. Kati ya lugha hizo, Kiitalia ndicho kinachofanana zaidi na Kilatini, labda baada ya Kisardinia.
Imegawanyika katika lahaja nyingi, hasa za Kaskazini na za Kusini mwa rasi hiyo. Imesanifiwa kwa msingi wa lahaja ya Firenze (mkoa wa Toscana, Italia ya Kati).
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Simone, Raffaele (2010). Enciclopedia dell'italiano. Treccani.
- Berloco, Fabrizio (2018). The Big Book of Italian Verbs: 900 Fully Conjugated Verbs in All Tenses. With IPA Transcription, 2nd Edition. Lengu. ISBN 9788894034813.
- Palermo, Massimo (2015). Linguistica italiana. Il Mulino. ISBN 9788815258847.